Darasani ticha anawafundisha madogo somo
la tabia njema. Ikafika muda wa kuwafundisha jinsi ya kuaga kwenda msalani kwa
haja ndogo wakati umekutana na binti kwa mara ya kwanza. Akaanza kuwauliza
madogo ajua kama wanajua jinsi ya kuaga au hawajui.
Akaanza: Haya, niambieni kama ndo
umekutana na msichana kwa mara ya
kwanza na mko mahali mnakula
ukashikwa na haja ghafla kwenda msalani utaaga vipi
Mjuni tusaidie.
Mjuni: Oya,
nisubiri dakika moja naenda chooni fasta narudi.
Ticha: No, hiyo
itakuwa ni kuhuni na inaonyesha kukosa nidhamu na kutojali.
Yes, Peter, wewe
ungesemaje?
Peter: samahani ila
nahitaji kwenda chooni mara moja nitarudi, sitachelewa.
Ticha: mh, hiyo ni
sawa ila bado si sahihi kutaja neno chooni na mko mezani mnakula.
Na wewe Joni
ungesemaje?
Joni: Ningesema,
mpenzi, naomba dakika chache, niwie radhi kuna rafiki yangu wa karibu sana
naenda kupeana naye mkono hapo nje, ambaye pia nina hakika angependa sana
kukusalimia siku moja kila kitu kikienda kadiri kilivyopangwa.
Ticha akaanguka chini akazimia!
Ticha akaanguka chini akazimia!
No comments:
Post a Comment