Kijana alipewa sharti la kunyoa nywele na
kusoma biblia kwa ufasaha akiweza hayo basi mdingi anamkabidhi gari kwakuwa
kijana tayari ana leseni.
Baada ya wiki kadhaa kijana akawa amewiva kwenye Baibo, na akamfuata mzee wake ili achukue gari akatanue. Hata hivyo hakutimiza sharti la kunyoa nywele. Katika kujitetea kwake kijana akasema:
"Baba katika kusoma kwangu Baibo , nimegundua watu muhimu wote kama Mussa na Samson hawakunyoa nywele, na kuna uwezakano mkubwa kuwa hata Yesu hakunyoa nywele. Hivyo nami sijataka nikuangushe baba yangu"
...Basi baba mtu akamjibu:-
" Natumaini pia ulisoma kuwa Mussa , Samson na Yesu hawakuwa wakitumia magari, walikuwa wakizunguka kwa miguu pande zote walizoenda, hivyo, swala la wewe kuwa na gari limeisha hapa".
No comments:
Post a Comment