Saturday, December 15, 2012

WENGINE HAMNAZO....

Jamaa alikuwa amechoka na kaz akaamua kufanya kituko ili apewe likizo au aambiwe akapumzike nyumbani.


Asubuhi ilipofika jamaa akaenda akajining‘iniza kwenye dali kama taa.



Bosi alipofika akashangaa na kuuliza 


‘unafanya nini huko juu??‘

Jamaa:mm ni taa namulika ofisi 


Bosi:naona kazi inakupa stress. nenda nyumbani ukapumzike.

Jamaa akashuka na kuanza ondoka na rafiki 

yake pale ofisini naye akainuka akamfuata nyuma.



Bosi akashangaa na kumuuliza rafiki 





‘na ww unaenda wapi??‘



Rafiki:sasa nitafanyaje kazi kwenye giza boss??



No comments:

Post a Comment