Tuesday, April 2, 2013

INSHA YA VITA

Mwalimu aliwaagiza wanafunzi wake waandike insha ya maneno 100 kila mmoja kuhusu vita ya Tanzania na Uganda kipindi cha Idd Amin. 

"Andika insha ya maneno yasiyozidi 100 ukiwa ni mwanajeshi katika vita vya Idd Amin wa Uganda na Tanzania kuanzia vita vinaanza hadi vilipoisha."

Wakati wa kusahihisha insha hizo mwalimu akakutana na insha ya
mwanafunzi mmoja aliyeandika:

"Yawaaaaaaaa! Uwiiiiiiii! Mama nakufaaaaaaaaaaa!!" Insha imeisha.

Mwalimu akamuita akamuuliza: mbona umeandika maneno machache hivi?


Mwanafunzi akajibu: yaani ile naingia tu vitani mpakani Kagera nikapigwa risasi hivyo sikumaliza vita.


No comments:

Post a Comment