Thursday, October 18, 2012

DOGO HAMNAZO

Ticha katoa assignment madogo wachore mchoro wowote mzuri kwenye karatasi nyeupe. Baada ya dakika 6 dogo mmoja akasimama kumpelekea ticha karatasi kwamba kamaliza. ticha kucheki akaona karatasi nyeupe dogo hajachora kitu. Akamswalika: 

Umechora nini?

Dogo: Sir nimechora ngo'ombe anakula majani.


Ticha: Sasa mbona hakuna majani hapa?


Dogo: Ng'ombe amekula yote sir!


Ticha: Na ng'ombe mwenyewe yuko wapi, mbona hakuna?


Dogo: Majani yalivyoisha na ng'ombe naye akaondoka sir, ndo maana hamna kitu!


No comments:

Post a Comment