Friday, November 9, 2012

VIOJA VYA INTERVIEW


Jamaa wawili Mbongo na Mkenya waliomba kazi katika post moja katika shirika  moja kubwa hapa nchini. Wote walikua na vigezo sawa kwaio mkuu wa kitengo akasema kwakua kuna nafasi moja na nyie wote mna vigezo sawa sasa itabidi niwape katest kidogo. Hivyo wakapewa kamtihani ka kuandika.

Baada ya kumaliza mtihani wote walipata maksi sawa na kulikosa swali moja katika kumi (10).

Mkuu wa kitengo akamfuata Mbongo na kumwambia,

“asante kwa kuonyesha interest ya kutaka kufanya kazi katika kampuni yetu, lakini ni Kwamba tumeamua kumpa kazi Mkenya”

Mbongo: (akastuka) 
“ kwanini iwe ivo il-hali wote tumepata maksi 9 sawa, hasa ukizingatia hapa ni Tanzania na mimi ni Mtanzania nilistahili nipate hiyo nafasi kwanini unampa mgeni??”

Mkuu wa Kitengo: 
“ni kweli wote mmepata maksi sawa, lakini uteuzi wetu haukutegemea maswali mliyojibu sahihi bali umetokana na lile swali ambalo wote mmekosa”

Mbongo: “ sasa apo ni kivipi majibu ya swali tulikosa, moja likawa afadhali kuliko lingine??”

Mkuu wa Kitengo:

“ rahisi sana, swali la 5, Mkenya kajibu “SIJUI” na wewe umejibu “HATA MIMI””

No comments:

Post a Comment