Tuesday, November 20, 2012

WAZEE HAWA KIBOKO


Msichana wa miaka 16 alipata  ujauzito. Wazazi wa binti walikasirika  sana baada ya kugundua. Mama wa  binti akaamua kumpa simu binti  yake aongee na aliyempa mimba ili
 akamfate aje naye. 

Baada ya nusu  saa binti aliondoka akarudi na  mwanaume ambaye alioneka ni  mzee wa makamo, huyo mzee  alikuja na gari nyekundu nzuri sana  akiwa na binti. Alipofika akaingia
 ndani akawasalimia wazazi na  kusema 

"samahani  sana wazazi kwani nimempa mimba  binti yenu na sitomuoa, ila kama  akijifungua mtoto wa kike nitawapa  kiwanda kimoja, ghorofa moja na Tsh  milioni mia mbili ila kama  akijifungua mtoto wa kiume  nitawapa viwanda viwili, ghorofa tatu  na Tsh milioni mia tano, ila ikitokea  mimba ikatoka sijui mngependa  nifanyaje? (akawauliza wazazi wa  binti) 

baba wa binti akajibu 

"apo  itabidi umpe mimba nyingine"

No comments:

Post a Comment