Monday, March 18, 2013

BWEGE FLANI

Kijana fulani alikuwa safarini, gari likamharibikia kijijini akaomba hifadhi katika nyumba moja akakaribishwa. Baada ya kuoga na kula:

Mzee mwenye nyumba: Sasa huyu mgeni sijui alale wapi?


Mama mwenye nyumba: Saa hizi ni usiku akalale na Bebi.

Jamaa kusikia jina Bebi akaona lazima huyu ni mtoto na labda anakojoa kitandani au analia akaona asije kumsumbua bure usiku.

Jamaa: Msipate tabu mi nitalala hapa hapa sebuleni kwenu.


Akalala.

Asubuhi wakati wanakunywa chai akaibuka msichana mmoja mrembo ajabu. Jamaa akapigwa na bumbuwazi karibu angejimwagia chai.

Binti: Umeamkaje mgeni? Naitwa Bebi, sijui wewe unaitwa nani?


Jamaa akajibu: aaaaaaaargghh!Mimi naitwa Mjinga bin Imekula Kwangu.


No comments:

Post a Comment