Thursday, May 17, 2012

JAMAA NA GARI JIPYA

Jamaa alikuwa kapaki gari lake jipya nje ya baa. 


Alipotoka kakuta mtu kaligonga na kukwangua rangi upande mmoja, ila akakuta kikaratasi kimewekwa kwenye kioo cha mbele, 


akafungua akakutwa kimeandikwa hivi…


"Mambo ndugu yangu? 
Watu walioniona nakwangua gari lako wananiangalia ninavyoandika hiki kikaratasi nadhani wanafikiri kuwa nakuachia anwani yangu, na namba ya simu ili ukija uweze kunipata nikulipe. 
Lakini hapa mjini mambo hayaendi hivyo, siku njema mkuu"



No comments:

Post a Comment