Thursday, May 10, 2012

WANASIASA NA UONGO...

 Wanasiasa 40 walipata ajali mbaya porini 


mkulima mmoja alikua akilima karibu na shamba hilo alipoona viel akasogea kutoa msaada...baada ya kuwakagua wote akaamua kuchimba shimo na kuwazika wote pamoja.


baada ya muda, polisi waliweza kufika kwenye eneo la tukio kwa kuchelewa sana kama kawaida yenu Bongo, walishangazwa sana walipofika na hawakuona hata maiti au majeruhi mmoja....


pembeni alikuwepo mkulima yule hivyo polisi wakamsogelea na kumuhoji nini kimetokea na mazungumzo yalikua hivi...


POLISI: Hebu tueleze imekuaje hapa mbona kunaajali na hakuna hata mwili mmoja au hata majeruhi wameenda wap??

MKULIMA: nimewazika wote na shimo lenyewe lile pale (akionyeshea mahali alipowazika).



POLISI: umewazika??..unahakika wote walikuwa wamekufa? 


MKULIMA: kuna wengine walikuwa wanalalamika kwamba hawajafa lakini si unajua wanasiasa walivyo waongo, mi nikajua tu wanadanganya nikawazika wote!!!

No comments:

Post a Comment