Thursday, February 7, 2013

JE NI KWELI??

Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia mumeo nakupenda lini?. 

Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu. 

Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;

Simu 1- Samahani nani mwenzangu?

Simu 2- He Mama Joji unaumwa?

Simu 3- Nami pia daima

Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?

Simu 5- Sijakuelewa una maana gani

Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe

Simu 8-Chukua taim yako

Simu 9-?!?

Simu 10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?

Simu 11 – Hivi naota?

Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu shenzi mkubwa

Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimi



No comments:

Post a Comment