Wednesday, February 27, 2013

TABIA NJEMA

Darasani ticha anawafundisha madogo somo la tabia njema. Ikafika muda wa kuwafundisha jinsi ya kuaga kwenda msalani kwa haja ndogo wakati umekutana na binti kwa mara ya kwanza. Akaanza kuwauliza madogo ajua kama wanajua jinsi ya kuaga au hawajui.

Akaanza: Haya, niambieni kama ndo umekutana na msichana kwa mara ya
kwanza na mko mahali mnakula ukashikwa na haja ghafla kwenda msalani utaaga vipi

Mjuni tusaidie.

Mjuni: Oya, nisubiri dakika moja naenda chooni fasta narudi.

Ticha: No, hiyo itakuwa ni kuhuni na inaonyesha kukosa nidhamu na kutojali.

Yes, Peter, wewe ungesemaje?

Peter: samahani ila nahitaji kwenda chooni mara moja nitarudi, sitachelewa.

Ticha: mh, hiyo ni sawa ila bado si sahihi kutaja neno chooni na mko mezani mnakula.

Na wewe Joni ungesemaje?

Joni: Ningesema, mpenzi, naomba dakika chache, niwie radhi kuna rafiki yangu wa karibu sana naenda kupeana naye mkono hapo nje, ambaye pia nina hakika angependa sana kukusalimia siku moja kila kitu kikienda kadiri kilivyopangwa. 

Ticha akaanguka chini akazimia!

No comments:

Post a Comment