Kuna jamaa watatu walifanya makosa makubwa saaana na wakaadhibiwa kifo. siku yao ya kufa walipelekwa hadi mahali pale walitakiwa wauwawe.
wakaambiwa ya kwamba kuna njia tatu unaweza ukafa na unaruhusiwa kuchagua yoyote katika hizi nazo ni
1. Kupigwa risasi ya kichwa na utakufa papo hapo
2. kunyongwa kwa ghafla na utakufa sekunde hiyohiyo
3. Upigwe sindano za virusi vingi vya UKIMWI na uendee uishi na upate mateso kisha ufe.
jamaa wa kwanza akasema mi nachagua kupigwa risasi.... basi mara moja akawekwa watu wakambutua akafa......
wa pili nae akaulizwa wachagua nini??
akajibu " dah bora mninyonge fasta tu nijifie"
basi bila kupoteza mda hata sekunde mbili hazijapita jamaa akafa
wa tatu akaulizwa na wewe je??
kwa kujiamini kabisa akasema mi nipigeni sindano za virusi....
jamaa wakashtuka... lakini wakaona haina neno mana walimpa chaguo basi wakamkandamiza sindano la kwanza la virusi vya UKIMWI....
wakati zoezi likiendelea jamaa alikua anacheka saaana tena kwa kujiamini hadi walipo maliza ndio akazidi kucheka saana..
wala wauwaji wakasema duh huyu jamaa vipi?? wakashauriana ngoja tumuongezee sindano nyingine..
wakamdunga ya pili
yaani mda huo jamaa ndio full kucheka kwa nguvu tena na kugala gala
ikabidi wamuhoji
"oyaa wee una matatizo gani?.... mzima kweli wewe??.... yaani tunakupiga sindano za UKIMWI lakini wapi ndio kwanza wacheka na kufurahi...... nini kinakufanya ucheke namna hiyo??"
jamaa akajibu
"yaani katika watu wajinga nimekutana nao duniani nyie ni namba moja.... mnanichoma sindano za UKIMWI wakati mie nimevaa Kondom hapa..... hahahahahaha sipati kitu""
jamaa wakaduwaaaa....
No comments:
Post a Comment