Kuna jamaa mmoja alikuwa kila siku usiku akilala anaota NGEDERE na PANYA wanacheza mpira ikabidi siku moja aende hospital kumuona dokta alipofika hospital mazungumzo yakawa hivi:-
JAMAA: "Dokta mimi nimekuja ninasumbuliwa na ndoto kila siku usiku nikilala naota Ngedere na Panya wanacheza mpira utanisaidiaje?"
DOKTA: "Kwa hilo tatizo lako ulilosema inabidi nikupe hizi dawa ukifika nyumbani uzimeze, ukizimeza kuanzia leo hauto ota tena ndoto hizo sawa!"
JAMAA: "Sawa dokta ila itabidi nianze kuzimeza kesho kwakuwa leo ndio Fainali nataka nijue nani atashinda katika mechi ya leo"
- Dokta alibaki anashangaa!
No comments:
Post a Comment