Tuesday, August 28, 2012

KAZIDIWA UJANJA....

jamaa mmoja alikua akiishi na mkewe, lakini mkewe alikua anafuga paka na yeye jamaa alikua hampendi kweli yule paka. siku moja akaamua aende akamtupe mbali.

akamchukua na kuendesha gari kama mtaa wa saba 7 mbele, akamuacha paka apo akaanza kurudi home, alipokua  anakaribia kwake akamuona paka naye anaingia ndani.. akashangaa kweli..akauchuna.

siku iliyofuata akamchukua paka na kumpeleka mbali zaidi kama mtaa wa 18 kutoka nyumbani kwake.. akumtupia apo ye akaanza kurudi nyumbani, alipokaribia nyumbani kwake akamuona tena paka naye amerudi anaingia ndani.... akapandwa na hasira...

kesho yake akaamka na kumchukua paka akaenda mbali zaidi akakata kushoto akakata kulia akanyoosha tena kushoto kulia akazunguka saaaana.. kisha akamtupa paka...... akaanza safari ya kurudi home...

baada ya muda akapiga simu kwa mkewe nyumbani

Jamaa: mke wangu vipi.... huyo paka yupo apo??

Mke: ndio mume wangu yupo katulia tu, vipi imekuaje??

Jamaa: hebu mpe simu anielekeze njia ya kurudi nyumbani...... maana mi nimepotea

No comments:

Post a Comment