Mpoki na Joti waliingia supamaketi, wakaanza kuzunguka na kuangalia vitu mbali mabali, wakiendelea kuwa bize wanaangalia Mpoki akaiba Chocolate 3 na kuficha pasipo kuonekana.
baadae walipotoka nje Mpoki akamwambia Joti
"aisee, mi ni noooma, huwezi amini nimeiba hizi chokoleti 3 na hakuna aliyeniona, we huniwezi kabisa"
Joti akasema
"aah, unataka uone mambo yangu, turudi supamaketi pale nikuonyeshe wizi wa ukweli "
wakarudi supamaketi na kuelekea kaunta wakamkuta muuzaji.
Joti akamuuliza
"unataka kuona mazingaombwe??"
muuza akajibu " ndio, onyesha"
Joti akasema
"nipe chokoleti moja"
akapewa, Joti akaila yoote
Joti akaomba tena nyingine, akapewa na kuila, kisha akaomba ya tatu akapewa na kuila.
kufika apo muuzaji akaona mmh nini kinaendelea ikabidi ahoji
"mazingaombwe yenyewe yako wapi mana unakula tu chokoleti""
Joti akamjibu
"angalia kwenye mifuko ya rafiki yangu utaziona chokoleti zako"
NANI MJANJA??
No comments:
Post a Comment