Siku moja simba aliamka akiwa amechoka sana na mning'inio kutoka na kazi ya usiku uliopita na shibe yake... sasa kutoka na kujisikia uchovu akaona ngoja aondoe uchovu fasta fasta akatoka uku akijitapa na kuunguruma kwa sauti ya juu....
mbele kidogo akamkuta Sungura.. akamuungurumia kwa sauti na kusema
"nani ni mnyama mkuu humu mbugani kooote???"
Sungura kwa sauti ya woga na kutetemeka akajibu
"ni wewe mfalme wetu wa nyika"
simbaa akaridhika akamuacha Sungura kisha akaendelea mbele, akakutana na mbwa mwitu kwa staili ile ile
"nakuuliza wewe, ni nani mnyama mkuu na mwenye mamlaka humu mbugani kwetu"
mbwa mwitu kwa kuufyata mkia na kutetemeka akajiu kwa sauti ya chini ni kigugumizi cha kulia
"ni,,,we..we mkuu na mfalme we tu nyika"
simba akazidi kujiona yuko safi zadi akasogea mbele akamkuta tembo akamkoromea tena
"wewe... nauliza ni nani mfalme na mkuu wa nyika yoote hii??"
tembo akakerwa na ule mkelele wa simba hivyo akamdaka simba na mkonge wake kisha akambamiza kwenye miti mara zaidi ya kumi na kumwaga chini, akampiga teke akajigonga kwenye mtu na kutua chini kisha akamsinya na guu lake
simba kwa sauti ya maumivu na ya kipooole kabisa akagumia maumivu "mmmmmh"
baada ya apo tembo akamuachia simba na kusepa zake
simba akajikongoja na kuinuka na kusema
"sasa na wewe kama hujui jibu la swali si ungeuchuna tu... ya nini kunibonda namna hii??"
No comments:
Post a Comment