Pasta 1: Tatizo langu mimi ni wizi, kila baada ya ibada lazima nikwapue sadaka za waumini, pls niombeeni kwa Mungu niache hii tabia.
Pasta 2: Tatizo langu mimi ni wanawake, kila mwanamke ninayemuona natamani kulala naye, inifakti nimelala karibu na waimbaji wote wa kike wa kwaya na wake za waumini. Pls pls niombeeni niachane na hii tabia.
Pasta wa tatu akaanza kulia.
Wenzake wakamuuliza wewe vipi?
Akajibu: Tatizo langu mimi ni umbea! Tukitoka tu hapa lazima nikaanze kutangaza kila kitu mlichosema. Niombeeni jamani hii tabia niiache!
Nani anahitaji kuombewa zaidi? Akili kumkichwa.
Nani anahitaji kuombewa zaidi? Akili kumkichwa.
No comments:
Post a Comment