Kuna muhindi mmoja alikua akisafiri na mkewe ambaye ni mjamzito na tumbo tayari lilikua kubwa tu linaloonekana bila kuhoji kwa njia ya treni. ndani ya hilo behewa pia kulikua na wanajeshi wa Kipakistani. kama inavyojulikana Wahindi na Wapakistani ni majirani na wanakaugomvi hivyo mara nyingi watu wa hizi nchi mbili wakikutana kila mmoja hupendi kumdhihaki mwenzie.
wale wanajeshi wakamuona yule Muhundi akiwa amejkaa na mkewe wakaona ngoja wakamzingua na kumtania. mmoja wao akasogea na kuanza kumuhoji.
Mjeshi: wee... vipi huyo mkeo ni mjamzito?? (ilhali akiona ile hali ya ujauzito)
huku wajeshi wenzake wakicheka
Muhindi: (kwa sauti ya kawaida, bila kujua jamaa anamzingua) ndio ni mjamzito, kama unavyomuona
Mjeshi: sasa akizaliwa mtoto wa kiume utapenda awe nani??
Muhindi: nitapenda awe Engineer
Mjeshi: (akicheka na wenzake) hahahaha.. enhe akiwa wa kike je??
Muhindi: nitapenda awe Daktari
Mjeshi: (akiendelea kucheka) haya sasa vipi azaliwe na asiwe wa kike au wa kiume??
wajeshi wenzie wakizidi kucheka
Muhindi ndio alipogundua kuwa hawa jamaa wanamsanifu nae akaona ngoja niwapatie..
Muhindi akajibu: nitapenda awe MWANAJESHI WA PAKISTANI
Wajeshi wa pakistani full hasira ila ndio hivyo hawakua na cha kumfanya
No comments:
Post a Comment