Friday, July 13, 2012

DOGO

DOGO:"Samahani,saa hizi saa ngapi?

BOUNCER:"Saa kumi na moja unusu."

DOGO:"Ok,Ikifika saa kumi na mbili kamili nitakushika tako."

BOUNCER:"Umesema nini we mtoto!"

Bouncer akaanza kumfukuza yule mtoto,baada ya mitaa miwili mtoto akaingia kwenye nyumba ya babu mmoja aliyekuwa amekaa nje anaota jua.
Bouncer nae akafika pale:

BOUNCER:"Babu nakitaka kile kitoto kilichokimbilia humu kwako."

BABU:"Kwani kuna nini unakifukuza hivyo."

BOUNCER:"Hiki kitoto kimesema eti ikifika saa kumi na mbili kamili kitanishika tako."

(Babu akaangalia saa yake)

BABU:"Sasa wasiwasi wako wa nini?....si saa kumi na mbili bado!"
.

No comments:

Post a Comment