Saturday, June 30, 2012

HILI BALAA

Jamaa mmoja ndani ya hoteli alipaza sauti na kusema 


"Manager wa hii hoteli yuko wapi?.....mke wangu anataka kujirusha dirishani afe." 


Manager akajibu "weee..kwanini?? haya mimi apa Sasa nikusaidie vipi mzee?"


Jamaa akajibu 


"We mshenzi nini! Leta funguo haraka nifungue dirisha, limefungwa!!"

MACHIZI WAWILI

Kulikua na machizi wawili wamepozi katika bustani ya hospitali ya vichaa wakiongea na kufurahi. daktari kuwaona vile akajua basi si ajabu wale wawili wameanza kupata nafuu akasogea awasikilize wanaongelea nini!:


Chizi 1: sahivi nina mipango mingi sana, hapa nimekaa napanga na kujua iweje!


Chizi 2: aaah hata mimi, ni vema tunapata mda tunatafakari! Vipi nini mpango wako?


Chizi 1: kwanza kabisa nataka ninunue hii dunia!


Chizi 2: aah ilo halitawezekana??


Apo daktari akaona huyu mmoja labda ana afadhali akaendelea kuwasikiliza


Chizi 1: wee kwanini nisiweze??


Chizi 2: mi siiuzi!!


Daktari hoi akaona apo hakuna afazali!!

USIFICHE TATIZO LAKO KWA MWENZI WAKO


Hii ilimtokea jamaa mmoja ambaye alikua na mpenzi wake na wakaja kuoana. Kila mmoja kumbe alikua na tatizo lake na amekua akilionea aibu hivyo hakuna aliyethubutu kuliweka wazi kwa mwenzie kwaio walikua wanajaribu na wanafanya kila mbinu kulificha ili mwingine asigundue.

Jamaa tatizo lake kubwa ilikua ni Kwamba akivaa viatu tu pale anapovua miguu yake inatoa harufu balaa…. Kwaio dawa yake ilikua akirudi tu anavua viatu na alikua na soksi maalumu anavaa papo apo so inapunguza ile makitu au havui soksi kabisa.

Vile vile mkewe akikua na tatizo la kunuka mdomo ile mbaya hasa anapolala tu pindi akiamka, hata alale kwa muda mfupi harufu yake inakua balaa kwaio dawa yake ilikua akiamka tu hasemi neno wala kupiga muayo anawahi bafuni na kupiga mswaki kurekebisha mambo.

Siku moja, kama kawaida yake jamaa kapiga mtungi yuko nduki balaa (kalewa) akarudi nyumbani kwake mishale ya saa 6 usiku. Akaingia ndani na kupitiliza kulala mana tungi lilizidi hivyo alishindwa kufanya zoezi lake la soksi. Akakuta mkewe amelala naye akajilaza na kupiga mbonji.

Ilipofika saa 10 na nusu alfajiri jamaa akastuka na pombe kidogo imekata kujipekua akakuta soksi moja hakuna na kale kaharufu anakasikia akaona duh hili soo…. Uku pombe ikiwa kichwani akaanza kuitafuta pasipo mafanikio.. la mwisho akaona hana jinsi bora amuamshe mkewe amuulize soksi yake iko wap..

Akaanza kumuamsha mkewe…

“weee…. Amka aisee kuna kitu nakitafuta sikioni”

Wakati huo mkewe usingizi umemkolea na kama ujua kausingizi ka ule mda kanakua katamu ukiamshwa unaona kero… akataka aitike ila akakumbuka duh akiitika tu ile harufu ya mdomo itatoka na litakua soo kwaio akauchuna.

Jamaa akaamsha tena si wajua kelele za mlevi zinavyoboa?

“wee mwanamke si nakuamsha mimi wajifanya umelala??....amkaa aisee”

Mwanamke kwa hasira akageuka akasema

“aaaaaaah…..nini??” mbele ya uso wa jamaa

Duh jamaa akakutana na ile harufu live…akastuka!!

“wee mwanamke duh…yani umekula soksi yangu???
Tema nakwambia tema!!!!”

ULEVI NI MATATIZO

Mlevi mmoja alipanda  daladala akakaa siti moja na mlokole.

Mlokole akasema


"mpendwa unajua unaenda motoni"


mlevi akapayuka


"konda nishushe kumbe huendi kariakoo"


Friday, June 29, 2012

ENZI HIZO NA RINGI LAKO


MATANGAZO MENGINE....


NGOMA IMEKOLEA


HAHAHA MDEBWEDO KWA KWELI


kwa hisani ya masanjawani....

MAMBO YA KUDAIWA… DAWA YA DENI ULIPE


Hii ilitokea live bila chenga kipindi kile mitandao ya simu za mezani imeanza. Ambapo ili uweze kuongea na mtu kulikua na operator anaye waunganisha kabla tekelinalokujia haija upugredi.

Joti alikau anadaiwa na Mpoki mda mrefu saana na akawa akimzungusha mno. Siku hiyo Mpoki akampigia simu Joti na Operator akawaunganisha na mazungumzo yalikua hivi:

MPOKI: hellow

JOTI: hallow

MPOKI: Mambo vipi Joti, mzima wewe? Mimi Mpoki…

JOTI: aah Mpoki kaka, salama kabisa vipi wewe mzima?

MPOKI: niko mzima haijambo familia? Wanaendeleaje?

JOTI: hawajambo kabisa sijui upande wako shemeji na watoto wazima?

MPOKI: wazima kabisa, sasa vipi lile deni langu utanilipa lini? Maana siku zina enda?

Kusikia vile Joti akaona hiki kimeo akajifanya hasikii..

JOTI: hallow?? Unasemaje sikusii fresh? Shiiiiiiiiiiiisssssssskwachakwacha 
(akiingiza makelele ya simu inayokatakata)
MPOKI: wee Joti vipi?

JOTI: Salama kaka, nambie?

MPOKI: hela yangu utanilipa lini??

JOTI: haloow….halooow haloow… sikusikii unasemaje??

Operator kuona vile ikabidi aingilie kati

OPERATOR: we Joti, hebu acha mchezo… mbona line iko clear kabisa na namsikia fresh??

JOTI: (Kwa hasira) kama unamsikia basi mlipe wewe!!!

Kisha akakata simu

MSAHAULIFU HUYU KIBOKO


Jamaa mmoja alikua na katatizo ka kusahau na hili lilimfanya awe anachanganya sana vitu.
Siku moja usahaulifu wake ulimfanya akaugulie hospitali:

DAKTARI: Hee wewe imekuaje tena umeungua ivo??

JAMAA: aaah dokta nilikua zangu hom napiga pasi sasa wakati naendelea simu yangu ikaita ssa nikajisahau baada ya kunyanyua simu nikainyanua pasi na kuweka sikioni ndio nikajiunguza namna hii.

Daktari akamgeuza kichwa kuchunguza akakuta masikio yote yameungua

DAKTARI: Aaah aisee pole sana… sasa mbona umeungua masikio yote mawili ilikua vipi?

JAMAA: baada ya kuungua upande mmoja nikakata simu....... Yule mshenzi si ndio akapiga tena......

Thursday, June 28, 2012

VURUGU LAKE KAMA NALIONA

Polisi mmoja wa traffic karudi home usiku kama saa 4 kuelekea saa 5 baada ya shift yake,ili asimuamushe mkewe hakuwasha taa ya chumbani kwake.

Akaanza kuvua uniform zake na kuzitundika.... alipotaka kusogea kitandani, ghafla mkewe akamwambia kwa sauti ya usingizi 

"Mpenzi usiwashe taa...kichwa kinaniuma vibaya naomba uende hapo jirani kwa duka la Omari ukaniletee panadol"

Polisi akavaa chapchap na kukimbia kwa Omari

POLISI:"Omari nipe panadol,mke wan
gu yu anaumwa na kichwa sana"

OMARI:"Hii hapa afande...he afande ulijiunga na kikosi cha magereza(prison) lini? Naona leo umevaa uniform ya magereza"

kilichofuata sikuwepo....

WATOTO WENGINE TABU....

BABA:"Tano ongeza kumi ni ngapi?"

MTOTO:"Sijui"

BABA:"Aaah we bwege,kwanini hujui hesabu rahisi ka hio!"

MTOTO:"Baba ukiona noti ya elfu 1 na ya mia 5 utaokota ipi?"

BABA:"Nitaokota ya elfu 1"

MTOTO:"We bwege,kwanini usiokote zote"


INTAVYUUUU

JOB INTERVIEW!

INTERVIEWER: Tell me the opposite of Good. 


MSELA: Bad.


INTERVIEWER: Come. 


MSELA : Go

INTERVIEWER: Ugly 


MSELA : Fine

INTERVIEWER: U're wrong!


MSELA : U're right! 

INTERVIEWER: Shut up! 


MSELA : Keep talking! 

INTERVIEWER: Ok now stop all that. 


MSELA : Ok now carry on all that. 


INTERVIEWER: Get out!


MSELA : Come in! 


INTERVIEWER: Oh my God. 


MSELA : Oh my Devil.


INTERVIEWER: U're Rejected.


MSELA : I'm selected...


WAKUMBUKA HII.....ULITUMIA NYOSHA MKONO JUU

HII NI VERE UKWELI

BURUDANI ZA WALEVI....

walevi wawili walikua wanapiga stori uku wakiendelea kilaji na kimewakolea.


wa kwanza anasema,


"jana niliota niko Marekani."


wa pili  naye anasema,


"mi niliota niko TBL mule ndani, nilikunywa pombe hadi nikaanza kumwaga zingine mana hawaruhusu kubeba nje"


wa kwanza akakasirika,


"we ni mbaya, mbona hukuniita."


wa pili akamjibu,


"nilikuja kwako mkeo akaniambia umeenda Marekani"



MMH HAPA SIJUI NINGEWAZAJE...!!

Enzi za ukoloni Wabongo wawili wakawa wa kwanza kupanda ndege, 


safari ya kuelekea Ulaya;


Mbongo 1: Aise hivi hii ndege ikizima huku juu itakuwaje?


Mbongo 2: Shhhhhh uchune, hawa wazungu hawana maana watatulazimisha tuisukume mpaka iwake.



HIZI POMBE HIZI...BALAA

Mlevi kafika kwake amelewa njwiiiiii.


Akawa anapata tabu kuingiza funguo kwenye kufuli la mlango wake,

 
jirani yake akaamuuliza unataka msaada,

 
akajibu,

 
'Tena sana jirani,hebu shikilia hii nyumba kila nikitaka kuingiza funguo nyumba inacheza'



ULEVI HUU HUU....!!!

Mlevi kapiga simu police


MLEVI;hello afande kuna wiz umetokea nimepaki gari kurudi nakuta haina sterring na siti ya dereva


AFANDE; okey, tunakuja sasa hivi, upo mtaa gani hapo au eneo gani??


MLEVI; "Oops? DUUH msije kumbe nimeingilia mlango wa nyuma"


Wednesday, June 27, 2012

IKUJE HII TSAILI SASA..EEH

AU NIMEIVA??

Mwendawazimu flani wa milembe alipanda juu mti wa mwembe asubuhi sana.


akakaa mtini hadi kitu saa kumi.


njaa ikamkaba mpaka penyewe.mara...chali akadondoka chini kutoka mtini.


daktari akaja akamwuliza 


"nini kimetendeka",


Mwendawazimu akajibu, 


"oyo usijali sana hata mi nashangaa au ndo kusema"NIMEIVA!"?

ESCAPE......

THINKING INSIDE THE BOX

SIJUI NDIO TAFSIRI YAKE...???






FULU MISIFA

Mpenda misifa mwenye Volkswagen yenye tint alikutana na jamaa mwenye Hammer kwenye kwenye trafic light.

Volkswagen: Oyaa gari lako lina simu?

Hammer: Ndio, we lako linayo?

Volkswagen: Yap. gari lako lina Kitanda?

Hammer: Hapana, lako je?

Volkswagen: Yap....taa zikawaka wakatimua. 

Jamaa mwenye Hammer akaona uchungu sana Kivolkswagen kiwe na kitanda gari lake halina, akaenda kufanya modification akatengeneza bonge ya kitanda, akaanza kumsaka mwenye volkswagen amkoge. Siku moja mapema akaiona Volkswagen imepaki madirisha yamefungwa, akagonga kioo, dreva wa Volkswagen akatoka.

Hammer: Unanikumbuka?

Volkswagen: Ndio kuna nini?

Hammer: Gari yangu ina dabo bed

Volkswagen: We chizi nini yaani umenitoa bafuni uniambie utumbo huo?

BAGIA ZINAISHA

Baba anamuuliza mwanae:


"He! Leo imekauaje?? alfajiri yote hii, mbona unawahi shuleni?"

MTOTO: mwalimu wa bagia leo anakuja asubuhi nikichelewa nitakuta zimeisha bure. 



BABA: pumbafu si kuwahi masomo bali bagia?

MTOTO: ndio si wanasema elimu haina mwisho? Lakini bagia zinaishaga! 



BABA: akaguna mh, hapa kazi ipö. 


(sijui kama wanaelewanaga na mwalimu wake..)

MSHUKURU MUNGU


ALAFU UNAJIFANYA KULALAMIKA...... GURUGUJA WEWE....!!

MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO..

NANI ALAUMIWE??

MZAZI:"Nikiwa na nazi 5 nikikupa 3 nitabaki na ngapi?"

CHALII:"Mi sijui"

MZAZI:"Aaah...kwanini hujui hesabu rahisi namna hii."

CHALII:"Shuleni huwa tunafundishwa hesabu za machungwa pekee"...


TUBEBE MIZIGO YETU

Ilikua Jumapili moja hivi...


jamaa karudi home kwake kutoka kanisani...kisha akamsalimu vizuri, akamnnyanyua mke wake na kumbeba kuzunguka nae ndani ya nyumba kisha akamtua chini.


mkewe kwa butwaa alilopata akahoji,


"uko kanisani leo padri kawafundisha kuhusu mapendo kwa wake zanu nini??"


jamaa akajibu,


"la hasha, padri amesema TUBEBE MIZIGO YETU"


Mkewe akafainti

VIOJA BARABARANI..


Hii imetokea juzi ruti ya kutoka Sinza kuelekea Posta mishale ya saa 3 asubuhi.

Kulikua na daladala imekula nyomi kama kawaida asubuhi kwenda town watu wanajaa tangu mwanzo wa basi kwa hiyo njiani kunakua hakuna haja ya kupakia tena……

Madereva wengi huamua kuchepuka na kupita vichochorni watokee magomeni kasha washushe jangwani, faya waingia mjini mapema wanede na kugeuka fasta.

Juzi dereva mmoja akafanya hivyo ili apite kama tandale uku aibuke magomeni kisha aenda town… kwa bahati mbaya  Trafiki walikuwepo alikopita akasimamishwa..

TRAFIKI: nyie ndio tunawatafuta siku zoote

DEREVA: kwanini muheshimiwa

TRAFIKI: mnajifanya mna haraka humu duniani kuliko watu wote sio??

DEREVA: hapana muheshimiwa ila hii gari imekodishwa kwa ajili ya harusi.

(abiria kwa nyuma wanasikilizia kinachoendelea)

TRAFIKI: (Aking’aka) aaah unanifanya mi zumbukuku sio… yani ndio wajizidishia makosa sasa gari linawekwa ndani na we mwenyewe dereva unaenda ndani(selo).

Abiria kusikia ivo, mmoja kwa nyuma akaanzisha,

…dada huyoo anaolewa…. Dada huyoo anaolewa.. 

(abiria wote wakaanza kuitikia)

Mahariiiii..... ishatolewaaa...  Dada huyooo anaolewa….dada huyooooo anaolewa….!!!

(trafiki akaona apo ameshindwa akaruhusu gari liendeleee…)

REMEMBER YOUR PAST





After eating, he gave 5$ to the waiter as a tip. The waiter had a strange feeling on his face after the tip.
Gates realized & asked. What happened?
Waiter: I'm just amazed Bcoz on the same table ur son gave Tip Of... 500$...
& u his Father, richest man in the world Only Gave 5$...?

Gates Smiled & Replied With Meaningful words:

"He is Son of the world's richest man, but i am the son of a wood cutter..."

( Never Forget Your Past. It's Your Best Teacher. )

KIPWINTO....

Jamaa kaingia kazini Jumatatu na macho yote mawili yamevimba kwa kipigo.

BOSS: Vipi tena mbona macho yamevimba umeanza ngumi siku hizi?


DEVI: Mkuu hapana mzee wema wangu umeniponza kwenye daladala asubuhi hii


BOSS: Kwani ilikuwaje?


DEVI: Nilikuwa kwenye daladala mbele yangu alikuweko amesimama mwanamke mnene, sinikaona gauni lake limeingia kwa bahati mbaya katikati ya makalio, nikaona nimsaidie kumhifadhi aibu nikainyofoa ile nguo kwa kuivuta taratibu, mshahara wake akageuga akanipiga ngumi ya jicho la kushoto


BOSS: Na jicho la kulia?


DEVI: Mzee nilipoona kakasirika nikajua basi hakupendezewa niitoe ile nguo, nikaona heri niirudishie ile nguo nilivyoikuta, akanitandika ngumi ya jicho la kulia


BOSS: Pole

UMESAHAU REMOTE..

Kibaka kaingia nyumba flani kaiba tv akaanza mbio uku kajitwisha tv

kumbe mle alipoiba kuna chizi likaanza kumfukuza,

kibaka kila akikata kona yule chizi anae tu wamekimbizana sana

Ikabidi kibaka asalimu amiri akasimama, mara yule chizi naye huyu hapa mbele ya kibaka 

Anamwambia

"Ulikua umesahau remote hii hapa chukua....."

Saturday, June 23, 2012

ENGLISH-SWAHILI DIKSHENARI

Direct translation from swahili to english

1.wacha mchezo-Leave sports

2.Mimi si mtu hivi hivi-Am not a person like this like this

3.Siku moja nitakutembelea-One day i will walk on you

4.Wewe ni kiboko yao-You are hippopotamus of them

5.Nasikia kizunguzungu-Am fealing english english

6.Uko macho-Are you eyes

7.U will go and water-utaenda na maji



8. Jamaa ni moto wa kuotea mbali - he is fire to dream from far


9. unanitafuta ubaya - u are searching me bad


10. nimesubiri nimesubiri lakini wapi - i waited i waited but where...


ongeza nawe tukuone..

mafundi kweli hawa??

On the gates of an engeneering shop, they wrote 


"We fix evrythng"

And on the door They wrote 



"Knock hard, the bell is not working".....!

haya mazungumzo kiboko

‎*Officer: What Is Your Name?

*Candidate: M P. Sir

*Officer: Tell Me Properly.

*Candidate: Mulenga PhIRI Sir

*Officer: Your Father’s Name?

*Candidate: M P. Sir

*Officer: What Does That Mean?

*Candidate: Monde PhIRI Sir

*Officer: Your Native Place

*Candidate: M P. Sir

*Officer: Is It Matero Police?

*Candidate: No, Matero Plots Sir

*Officer: What Is Your Qualification?

*Candidate: M P. Sir

*Officer: (angrily) What Is It?

*Candidate: Metric Pass 


*Officer:so why do you need a job?

*Candidate:M P sir

*Officer:meaning?

*Candidate: Money Problem sir

*Officer:whats your personality?

*Candidate:MP sir

*Officer:would you explain yourself and stop wasting my time?

*Candidate: Monacrotic Personality

*Officer: I see. I will get back to you

*Candidate:so sir, how's my MP?

*Officer:and whats that again?

*Candidate: My Performance

*Officer: MP!!!

*Candidate: meaning?

*Officer:MP - Mental Problem!