Thursday, June 28, 2012

VURUGU LAKE KAMA NALIONA

Polisi mmoja wa traffic karudi home usiku kama saa 4 kuelekea saa 5 baada ya shift yake,ili asimuamushe mkewe hakuwasha taa ya chumbani kwake.

Akaanza kuvua uniform zake na kuzitundika.... alipotaka kusogea kitandani, ghafla mkewe akamwambia kwa sauti ya usingizi 

"Mpenzi usiwashe taa...kichwa kinaniuma vibaya naomba uende hapo jirani kwa duka la Omari ukaniletee panadol"

Polisi akavaa chapchap na kukimbia kwa Omari

POLISI:"Omari nipe panadol,mke wan
gu yu anaumwa na kichwa sana"

OMARI:"Hii hapa afande...he afande ulijiunga na kikosi cha magereza(prison) lini? Naona leo umevaa uniform ya magereza"

kilichofuata sikuwepo....

No comments:

Post a Comment