Mpenda misifa mwenye Volkswagen
yenye tint alikutana na jamaa
mwenye Hammer kwenye kwenye trafic light.
Volkswagen: Oyaa gari lako lina simu?
Hammer: Ndio, we lako linayo?
Volkswagen: Yap. gari lako lina Kitanda?
Hammer: Hapana, lako je?
Volkswagen: Yap....taa zikawaka wakatimua.
Jamaa mwenye Hammer akaona uchungu sana
Kivolkswagen kiwe na kitanda gari lake halina, akaenda
kufanya modification akatengeneza bonge ya kitanda, akaanza
kumsaka mwenye volkswagen amkoge. Siku moja mapema
akaiona Volkswagen imepaki madirisha yamefungwa, akagonga
kioo, dreva wa Volkswagen akatoka.
Hammer: Unanikumbuka?
Volkswagen: Ndio kuna nini?
Hammer: Gari yangu ina dabo bed
Volkswagen: We chizi nini yaani umenitoa bafuni uniambie utumbo huo?
No comments:
Post a Comment