Hii ilimtokea jamaa mmoja ambaye alikua na mpenzi wake na
wakaja kuoana. Kila mmoja kumbe alikua na tatizo lake na amekua akilionea aibu
hivyo hakuna aliyethubutu kuliweka wazi kwa mwenzie kwaio walikua wanajaribu na
wanafanya kila mbinu kulificha ili mwingine asigundue.
Jamaa tatizo lake kubwa ilikua ni Kwamba akivaa viatu tu
pale anapovua miguu yake inatoa harufu balaa…. Kwaio dawa yake ilikua akirudi
tu anavua viatu na alikua na soksi maalumu anavaa papo apo so inapunguza ile
makitu au havui soksi kabisa.
Vile vile mkewe akikua na tatizo la kunuka mdomo ile mbaya
hasa anapolala tu pindi akiamka, hata alale kwa muda mfupi harufu yake inakua
balaa kwaio dawa yake ilikua akiamka tu hasemi neno wala kupiga muayo anawahi
bafuni na kupiga mswaki kurekebisha mambo.
Siku moja, kama kawaida yake jamaa kapiga mtungi yuko nduki
balaa (kalewa) akarudi nyumbani kwake mishale ya saa 6 usiku. Akaingia ndani na
kupitiliza kulala mana tungi lilizidi hivyo alishindwa kufanya zoezi lake la
soksi. Akakuta mkewe amelala naye akajilaza na kupiga mbonji.
Ilipofika saa 10 na nusu alfajiri jamaa akastuka na pombe
kidogo imekata kujipekua akakuta soksi moja hakuna na kale kaharufu anakasikia
akaona duh hili soo…. Uku pombe ikiwa kichwani akaanza kuitafuta pasipo
mafanikio.. la mwisho akaona hana jinsi bora amuamshe mkewe amuulize soksi yake
iko wap..
Akaanza kumuamsha mkewe…
“weee…. Amka aisee kuna kitu nakitafuta sikioni”
Wakati huo mkewe usingizi umemkolea na kama ujua kausingizi
ka ule mda kanakua katamu ukiamshwa unaona kero… akataka aitike ila akakumbuka
duh akiitika tu ile harufu ya mdomo itatoka na litakua soo kwaio akauchuna.
Jamaa akaamsha tena si wajua kelele za mlevi zinavyoboa?
“wee mwanamke si nakuamsha mimi wajifanya
umelala??....amkaa aisee”
Mwanamke kwa hasira akageuka akasema
“aaaaaaah…..nini??” mbele ya uso wa jamaa
Duh jamaa akakutana na ile harufu live…akastuka!!
“wee mwanamke duh…yani umekula soksi yangu???
Tema nakwambia tema!!!!”
HE HE HE VITUKO MAJANGA MIX
ReplyDelete