Jamaa kaingia kazini Jumatatu na macho yote mawili yamevimba kwa kipigo.
BOSS: Vipi tena mbona macho yamevimba umeanza ngumi siku hizi?
DEVI: Mkuu hapana mzee wema wangu umeniponza kwenye daladala asubuhi hii
BOSS: Kwani ilikuwaje?
DEVI: Nilikuwa kwenye daladala mbele yangu alikuweko amesimama mwanamke mnene, sinikaona gauni lake limeingia kwa bahati mbaya katikati ya makalio, nikaona nimsaidie kumhifadhi aibu nikainyofoa ile nguo kwa kuivuta taratibu, mshahara wake akageuga akanipiga ngumi ya jicho la kushoto
BOSS: Na jicho la kulia?
DEVI: Mzee nilipoona kakasirika nikajua basi hakupendezewa niitoe ile nguo, nikaona heri niirudishie ile nguo nilivyoikuta, akanitandika ngumi ya jicho la kulia
BOSS: Pole
No comments:
Post a Comment