Thursday, June 21, 2012

JAMAA MUONGO HUYU...

Mvuta bhangi flani muongo aliondoka mtaani kwa mwezi mmoja.

Aliporudi mtaani akaanza kusema alikuwa Dubai.
Wavuta bhangi wenzake wakamuuliza kama aliona lile jumba refu zaidi ya yote duniani.

Akajibu "Eeeh nilifika mpaka hapo kukawa na mwarabu mmoja mpuuzi aliyejirusha kutoka kilele mwa hiyo nyumba."

Wenziwe wakamwambia "Duh kweli huyo ni mpuuzi,alikufa ama kaponea...?

Jamaa akadakia "Alikufa!! Siku tatu yuko hewani bila chakula.....utaponea kweli hapo"


1 comment:

  1. Aiseeeee.....siku tatu hewani gravity ilizmwa nini!!!!!

    ReplyDelete