Friday, June 29, 2012

MSAHAULIFU HUYU KIBOKO


Jamaa mmoja alikua na katatizo ka kusahau na hili lilimfanya awe anachanganya sana vitu.
Siku moja usahaulifu wake ulimfanya akaugulie hospitali:

DAKTARI: Hee wewe imekuaje tena umeungua ivo??

JAMAA: aaah dokta nilikua zangu hom napiga pasi sasa wakati naendelea simu yangu ikaita ssa nikajisahau baada ya kunyanyua simu nikainyanua pasi na kuweka sikioni ndio nikajiunguza namna hii.

Daktari akamgeuza kichwa kuchunguza akakuta masikio yote yameungua

DAKTARI: Aaah aisee pole sana… sasa mbona umeungua masikio yote mawili ilikua vipi?

JAMAA: baada ya kuungua upande mmoja nikakata simu....... Yule mshenzi si ndio akapiga tena......

No comments:

Post a Comment