Hii ilitokea live bila chenga kipindi kile mitandao ya simu za mezani
imeanza. Ambapo ili uweze kuongea na mtu kulikua na operator anaye waunganisha
kabla tekelinalokujia haija upugredi.
Joti alikau anadaiwa na Mpoki mda mrefu saana na akawa akimzungusha mno. Siku
hiyo Mpoki akampigia simu Joti na Operator akawaunganisha na mazungumzo yalikua
hivi:
MPOKI: hellow
JOTI: hallow
MPOKI: Mambo vipi Joti, mzima wewe? Mimi Mpoki…
JOTI: aah Mpoki kaka, salama kabisa vipi wewe mzima?
MPOKI: niko mzima haijambo familia? Wanaendeleaje?
JOTI: hawajambo kabisa sijui upande wako shemeji na watoto wazima?
MPOKI: wazima kabisa, sasa vipi lile deni langu
utanilipa lini? Maana siku zina enda?
Kusikia vile Joti akaona hiki kimeo akajifanya hasikii..
JOTI: hallow?? Unasemaje sikusii fresh? Shiiiiiiiiiiiisssssssskwachakwacha
(akiingiza
makelele ya simu inayokatakata)
MPOKI: wee Joti vipi?
JOTI: Salama kaka, nambie?
MPOKI: hela yangu utanilipa lini??
JOTI: haloow….halooow haloow… sikusikii unasemaje??
Operator kuona vile ikabidi aingilie kati
OPERATOR: we Joti, hebu acha mchezo… mbona line iko clear kabisa na
namsikia fresh??
JOTI: (Kwa hasira) kama unamsikia basi mlipe wewe!!!
Kisha akakata simu
No comments:
Post a Comment