Saturday, June 30, 2012

MACHIZI WAWILI

Kulikua na machizi wawili wamepozi katika bustani ya hospitali ya vichaa wakiongea na kufurahi. daktari kuwaona vile akajua basi si ajabu wale wawili wameanza kupata nafuu akasogea awasikilize wanaongelea nini!:


Chizi 1: sahivi nina mipango mingi sana, hapa nimekaa napanga na kujua iweje!


Chizi 2: aaah hata mimi, ni vema tunapata mda tunatafakari! Vipi nini mpango wako?


Chizi 1: kwanza kabisa nataka ninunue hii dunia!


Chizi 2: aah ilo halitawezekana??


Apo daktari akaona huyu mmoja labda ana afadhali akaendelea kuwasikiliza


Chizi 1: wee kwanini nisiweze??


Chizi 2: mi siiuzi!!


Daktari hoi akaona apo hakuna afazali!!

No comments:

Post a Comment