Hii imetokea juzi ruti
ya kutoka Sinza kuelekea Posta mishale ya saa 3 asubuhi.
Kulikua na daladala
imekula nyomi kama kawaida asubuhi kwenda town watu wanajaa tangu mwanzo wa
basi kwa hiyo njiani kunakua hakuna haja ya kupakia tena……
Madereva wengi huamua
kuchepuka na kupita vichochorni watokee magomeni kasha washushe jangwani, faya
waingia mjini mapema wanede na kugeuka fasta.
Juzi dereva mmoja
akafanya hivyo ili apite kama tandale uku aibuke magomeni kisha aenda town… kwa
bahati mbaya Trafiki walikuwepo
alikopita akasimamishwa..
TRAFIKI: nyie ndio
tunawatafuta siku zoote
DEREVA: kwanini
muheshimiwa
TRAFIKI: mnajifanya
mna haraka humu duniani kuliko watu wote sio??
DEREVA: hapana muheshimiwa
ila hii gari imekodishwa kwa ajili ya harusi.
(abiria kwa nyuma
wanasikilizia kinachoendelea)
TRAFIKI: (Aking’aka)
aaah unanifanya mi zumbukuku sio… yani ndio wajizidishia makosa sasa gari
linawekwa ndani na we mwenyewe dereva unaenda ndani(selo).
Abiria kusikia ivo,
mmoja kwa nyuma akaanzisha,
…dada huyoo anaolewa….
Dada huyoo anaolewa..
(abiria wote wakaanza
kuitikia)
Mahariiiii..... ishatolewaaa... Dada huyooo anaolewa….dada
huyooooo anaolewa….!!!
(trafiki akaona apo
ameshindwa akaruhusu gari liendeleee…)
KIJANA KALEYA,HAYA BANAAAA
ReplyDelete