Jamaa mmoja
alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani waliona uyoga,
wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini
kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza kuwa
si uyoga wa kula.
Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.
Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.
Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa.
Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.
Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.
Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nani nitubu Kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si wakon nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.
Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani.
Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani na kukuta wakigombana. Akawauliza ,Baba na mama mnagombania nini humu ndani,badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule nje?
Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.
Fikiria ni wewe ITAKUWAJE?
No comments:
Post a Comment