Sunday, July 29, 2012

UJANJA WA UKWELI



Dogo mmoja alipata nafasi ya kufanya Field katika kampuni moja sana kubwa hapa nchini. 


siku moja akiwa anaendelea na kazi... akapiga simu jikoni nakuanza kufoka..


"we mpuuzi yaani mda wote huo mi nimekaa apa nasubiri chai tu na hujaleta hadi sasa hivi.....nyambafu"


Upande wa pili ukajibu kwa hasira


"wee mpumbavu nini, unajua unaongea na nani??"


dogo akashtuka... (kucheki kapiga wrong extension number).... akajibu 


"sijui"


upande wa pili ukajibu


"unaongea na Managing Director wa kampuni hapa...shenz mkubwa wewe."


dogo akaona duh sasa huo msala, akajikakamua na yeye akajibu kwa kufoka


"na wewe unajua unaongea na nani??"


Upande wa pili ukajibu


"sijui"


dogo akashusha pumzi na kusema 


"duh afadhali....asante Mungu"


akakata simu.





No comments:

Post a Comment