Friday, July 20, 2012

UMENIIBIA

Joti kaenda dukani (aliponunua redio siku mbili zilizopita) akilalamika... muuzaji alikua Masanja


Joti: aaah ndugu yangu hata sijategema ungeniibia....?? yaani siamini!!


Masanja:  (akamkumbuka alimuuzia redio siku 2 zilizopita) kukuibia tena ndugu yangu?? hapana mi siwezi kufanya ivo!!


Joti: ndio tena usijifanye huelewi naongea nini?


Masanja: hapana ndugu yangu mi hii ndio biashara yangu na kipato changu nategemea hapa kwahiyo siwezi kufanya uhuni namna hiyo.... mbona nimekuuzia redio safi sana tena jenuini??


Joti: hakuna sio jenuini.......mi nimeisoma mwenyewe redio imeandikwa Made in Japan mbona kila nikisikiliza inasema "Unasikiliza Redio Tanzania"


Masanja na baadhi ya wateja hoi kwa kicheko....

No comments:

Post a Comment