Wednesday, July 11, 2012

HUYO MTOTO NI NANI???

Vengu alimuita Masanja kisha akamuuliza....


"wazazi wangu wana mtoto... na huyo mtoto sio dada yangu na wala sio kaka yangu... je huyo mtoto ni nani??"


masanja akafikiria na kufikiria kisha akaona hana ujanja akamjibu


" dah....mi sijui kwa kweli..jibu lake ni nini??"


Vengu akacheka...


" hahahaha...jibu lake ni mimi ndio huyo mtoto"


Masanja baada ya apo akaondoka zake akaona dah kumbe swali lilikua rahisi namna ile akaona ngoja nae akampate wa kwake kumuuliza.... akamfuata Mpoki.


Masanja: "Mpoki eeeh..... kuna swali apa"


Mpoki: (kwa majigambo kama kawa) "Uliza tu hakuna nitakachoshindwa"


Masanja: " wazazi wangu wana mtoto.... na huyo mtoto sio kaka yangu na wala sio dada yangu....Je huyo mtoto ni nani??"


Mpoki aawazaaa na kufikiri pasuipo kupata jibu akamwambia masanja


"hebu ngoja kidogo"


Mpoki akamfuata Joti


Mpoki: "Joti eeh..... kuna swali apa...eti wazazi wako wana mtoto na huto mtoto sio kaka yako na wala sio dada yako je huyo mtoto ni nani??"


Joti: (kicheko cha kimdobwedo) "hahahahaha yakhee.... kweli we hamnazo... misifa yote hujui ilo??"


Mpoki: "aaah sasa kejeli za nini si unipe jibu kama wajua??"


Joti: "Jibu lake ni mimi"


Mpoki akafurahi na baada ya apo akatoka nduki kurudi kwa Masanja akasema (kwa kujiamini)


" kaswali kako karahisi nimekapatia jibu"


Masanja: " haya sema jibu lake nini?"


Mpoki: "huyo mtoto ni Joti"


Masanja: (akacheeka) " hahahahahaha umekosaaaaaaa....mwanawane""


Mpoki:....( kwa mshangao): " aaah kivipi sasa??"


Masanja: "jibu lake, huyo mtoto ni Vengu"

No comments:

Post a Comment