Thursday, July 12, 2012

ULEVI NI KIMEO

Walevi watatu walikodi taxi usiku toka baa moja Dar kuelekea baa ya Kibaha. 


Dereva Taxi baada ya kuchtukia akawafanyia mchezo achukue hela bila kutumia nguvu! 


Basi akawasha gari kwa dakika 3 halafu akaizima na kuwaambia walevi 


"tayari tumefika Kibaha!" 


Mlevi wa kwanza akatoa pesa elfu 45 na kulipa.


Wa pili akachuka akisema 


"Asante dereva." 


wa tatu baada ya kushuka akaenda hadi mlango wa dereva taxi na kuufungua kisha kimzaba boonge la kibao!


Dereva taxi akaona mbinu yake imegundulika na tayari yuko matatani! 


Lakini yule mlevi aliyemnasa kibao akasema


 "Siku nyingine usiendeshe gari kama Shumaiko!!Ulitaka kutuua?!?!"


(Kwa hisani ya Sekioni "Seki")

No comments:

Post a Comment