Siku ya kufunga shule mzazi mmoja kaenda na mwanae shule,sherehe zikaanza wanafunzi wakawa wanapewa vyeti na zawadi kadri ya uwezo wao.
Mtoto wa jamaa yetu hakutajwa hata jina.
Mzazi akaangalia wale watoto waliofanya vizuri akamwambia mwanawe,
BABA:"Wale sasa ndio watoto,mbona mungu kaninyima."
Wakaondoka na kuelekea kituo cha basi kuwahi basi la kuenda kwao.Wakati huo huo wazazi kadhaa wenye magari wakawa wanachukua watoto wao.Mtoto akaangalia wale wazazi na kumwambia babake
MTOTO:"Wale sasa ndio wazazi mbona mungu kaninyima."
nyc
ReplyDelete