Tuesday, July 3, 2012

MAPENZI KIBOKO


Kulikua na jamaa mmoja alikua anampenda saana demu mmoja hivi ila tatizo alikua anaogopa kumweleza kwa Bahati nzuri alikua akiwasiliana nae kwa simu ila kikawaida. Akashindwa kabisa kumwambia kuwa anampenda.

Siku moja aakaamua kujitoa muhanga, akiwa hom anajiandaa kulala akaanda msg kumtumia Yule mrembo.

Akaandika “I LOVE YOU” na kuituma msg

Kisha akaweka simu pembeni asitake kusoma kama kutakua na ujumbe umerudi mana alikua akihofia ni jibu gani atapewa…basi kwa woga na kutetemeka akajitahidi mpaka akalala, baada ya mda akasikia mlio wa simu ukiashiria kuna msg mpya akajipa moyo at least kajibiwa hivyo jibu litakua zuri, akaona bora alale kisha asubuhi aisome msg iwe kama surprise kwake kwa jibu atakalo pewa..

Ilipofika asubuhi akafungua simu ili asome ujumbe aliojibiwa..ile kufungua akakutana na surprise ya kutosha,,wajua ni ujumbe gani??

Hehehehe wataka kujua??

Ona ni huu……..

“NDUGU MTEJA, TUNASIKITIKA YA KWAMBA HUNA SALIO LA KUTOSHA KUWEZA KUFANYA HUDUMA HII, TAFADHALI ONGEZA SALIO LAKO, tiGO EXPRESS YOURSELF”

No comments:

Post a Comment