Thursday, July 5, 2012

VIOJA HOTELINI


Jamaa kaenda kwa hoteli na kuagiza msosi..wali maharage na nyama… alipoanza kula akakutana na jiwe la kwanza…kidogo la pili…mara la tatu…..akaita muhudumu

Jamaa: we muhudumu hebu njoo apa..

Mhudumu: nimekuja ndugu mteja nini tatizo??

Jamaa: mbona chakula chenu kinakua hivi kinaiva nusu nusu tu??

Muhudumu: samahani sijakuelewa unamaanisha nini Kwamba kimeiva nusu?

Jamaa: mawe kwenye wali hayajaiva…

(WATEJA WENGINE HOI KWA VICHEKO.... JAPO KASEMA JAMBO LA UKWELI)

1 comment: