Jamaa kasimamishwa na trafiki yuko hai spidi mwanawani. Sasa ona maongezi:
Trafiki: Unajua kuendesha kasi kiasi hicho ni kosa la jinai?
Jamaa: Najua lakini wala sijali, kwani we unatakaje?
Trafiki: Khaa, hebu nipe kadi yako ya gari.
Jamaa: Kadi sina, kwanza hili gari nimeliiba muda is mrefu.
Trafiki: Unasema?! Kwa hiyo wewe ni jambazi na inaelekea unatumia silaha!
Jamaa: Sio silaha nyingi, Shoti Gani, AK47, risasi mia 300 na mabomu machache ya kutupa kwa mkono. Pia nina kiroba cha bangi.
Trafiki: Leo umekwenda na maji mwanaharamu wewe. Fungua buti la gari nikague.
Jamaa: Sitaki, kuna vichwa 20 ya watu kwenye buti kwa ajili ya kutoa sadaka. Na kuna watu wawili nimewaua naenda kuwatupa, pia wako humo kwenye buti.
Trafiki: Mungu wangu!!!!!! Hai spidi, gari umeiba, unamiliki silaha, muuaji, leo ndo mwisho wako.
Afande kakamata simu kampigia Ze Bigi Bosi Kova mwanawane. Ngrriiiiiiiiiiiiiii. Afande nimekamata jambazi sugu ana vichwa 20 vya binadamu, kaiba gari, kaua, ana silaha na madawa ya kulevya.
Mwanawane madifenda hayo na Kova ndani vyuuuuuupu eneo la tukio.
Kova: Fungua buti usachiwe.
Jamaa akafungua. Kova: Mbona hamna vichwa wala hamna hao watu, wala madawa?
Jamaa: Afande Kova, mimi hata nashindwa kuelewa askari wetu siku hizi wamekuwaje. Hapo nahisi atakuwa pia amekudanganya kwamba nina silaha na nilikuwa hai spidi. Ndo kawaida kutubambikia.!
Mwanawane, jamaa huyooooooo akaachiwa asepe zake!
No comments:
Post a Comment