Watoto
wengine kimeo
Joti
karudi nyumbani siku hiyo akitokea shule huku akiruka ruka na kuimba na kucheza…
baba yake, Mpoki, kumuona vile akashangaa, mbona leo dogo anarudi akiwa na
furaha namna iyo na haiwi ivo siku zote?
Mpoki
akamuuliza
“eeeh mwanangu imekuaje leo umekua na furaha namna hiyo kuliko siku
zote na hata sijawahi kukushuhudia ukiwa namna iyo??...vipi kuna nini
mwanangu??”
Joti
akajibu
“aisee
baba, mwaka huu wala hautahangaika kuninunulia vitabu vipya, madaftari mapya na
vingine kama hivo..kwa mwaka mzima”
Mpoki
akafurahi akasema
“ aaa aisee safi sana mwanangu, yani ndio mana nakupenda….."
(gafla
akashtuka, akahoji)
“hebu
ngoja kwanza…………………….. kwanini unasema sitanunua hivyo vyote umefanyaje
mwanangu??”
Joti
akajibu kwa kujiamini
“aaaah
si nimerudia darasa lile lile baba...”
No comments:
Post a Comment