mmarekani na mbongo walkuwa wakisafiri katika ndege na safari ilikua ndefu ya zaidi ya masaa 8, mmarekani akaona apoteze mda hivyo mmarekani akataka kumuonesha mbongo, kuwa wazungu wanaakili sana....
akawa anamuulza maswali ya kijinga mbongo. mbongo kuona anaznguliwa akaamua kumpotezea, mana alikua amechoka na angependa alale apumzike lakini mmarekani akawa anasisitiza.
mmarekani akatoa wazo basi wacheze mchezo wa maswali, akamwambia mbongo kuwa waulizane maswali na iwapo mbongo atashindwa kujibu ampatie mzungu dola 5 na iwapo mbongo atauliza swali na mzungu atashindwa kujibu basi mzungu ampatie mbongo dola 500. hii yote ilimradi mbongo asilale na wawepo wote kuupoteza mda.
mbongo akaona hapo ndo pakumlia na kumkomesha mmarekani. maswali yakaanza hivi
mzungu; rais wa tano wa USA anaitwa nan?
Mbongo hakuwa na jibu akatoa dola 5 akampa mzungu.
mzungu akacheka sana kisha akampa jibu
mbongo akauliza; ni kitu gani kinachopanda juu na miguu minne kisha kinarudi na mitatu?
Mzungu akawaza akafungua google, wikipedia, akawatumia rafiki zake mail lakini hakuna aliyekuwa na jibu.
baada ya masaa mawili akamuamsha mbongo aliyekuwa kapitiwa usingiz na kumpatia dola 500.
mbongo akapokea,akacheka kisha akarudi kulala
mzungu akamuuliza kwa ukali
"mpumbavu we mbona haujanipa jibu? ni kitu gani kinapanda juu na miguu minne kinashuka na mitatu?"
mbongo akatoa dola 5 akampa mzungu kisha akalala tena
Mzungu; "kenge mkubwa umeuliza swali ambalo haujui!"
No comments:
Post a Comment