Monday, July 23, 2012

ALIONGEZWA MSHAHARA WE CHEKI ILIKUAJE??


Da Kiboga ambaye ni  house girl aliomba aongezwe mshahara.

mama mwenye nyumba akasikitika sana kwa kitendo hicho mana hakuamini kwa jinsi alivyomlea Kiboga na kumpenda kama mtoto wake itatokea siku atasema hivyo. hivyo ikabidi amuulize.

Mama: sasa Kiboga, ni kwanini unasema hivyo wataka uongezewe mshahara, kwa sababu zipi za msingi??

Kiboga: mama, kwa kweli nina sababu tatu 3 za msingi kwanini ninahitaji uniongeze mshahara.

"kwanza, mimi naweza kunyoosha nguo zaidi yako?"

Madam: "eeeh! na ni nani kakwambia hivo??"

Kiboga: Baba kasema hivyo

apo mama akawa mdogo akaitikia tu

Kiboga: "Pili, naweza kupiga zaidi yako"

Mama: "sasa Kiboga naona unaleta upuuzi, nani kakudanganya unaweza kupika zaidi yangu nami ndio nimekufundisha??"

Kiboga: "baba huyo kasema"

dah apo mama akazidi kuwa mdogo, akauliza

"ya tatu je?"

Kiboga: " mi ni zaidi yako kwenye mapenzi pia"

apo mama akili ikamruka uwiiiii...kwa unyoonge kabisa..!!

Mama: "na hiyo ni baba amesema??"

Kiboga: "hapana mama sio baba, dereva ndio kaniambia hivyo"

NAKWAMBIA DA KIBOGA ALIPEWA ONGEZO LA MSHAHARA KULIKO HATA ALIVOTEGEMEA.....




No comments:

Post a Comment