Ukiambiwa
pombe ni kimeo kazima ukubali….. hasa ikimzidi mtu!
Hawa walevi
wana vituko sana mana wakishalewa tu hujiamini na wanaona kila kitu ni sahihi
kwao…unaweza kujiuliza inakuaje mtu anakua namna ile…hebu msikie huyu….
Jamaa
alikua amelewa sana, wakati anadrive kurudi mahome kwake njiani akasimamishwa
na trafiki….ona ilivokua!
TRAFIKI:
habari yako?
MLEVI:
(kwa sauti ya kilevi) niko pouwa kabisa…nini shida yako!?
TRAFIKI:
(akastuka kuwa jamaa kalewa mbaya) wee hebu shuka chini??
MLEVI:
aaah mi nimelewa sana siwezi hata simama kama vipi we ingia ndani!!
Trafiki
hoi hakuamini…
TRAFIKI:
waendesha huku umelewa, hebu twende kituoni!
MLEVI:
hapana mzee, mi naenda home saivi sielekei uko…kama unataka lifti panda hutaki
mi natembea….! (vuuum akiwasha gari na kuondoka)
Trafiki
alishindwa hata kuchukua namba ya gari kwa mshangao!
No comments:
Post a Comment