Wednesday, June 27, 2012

FULU MISIFA

Mpenda misifa mwenye Volkswagen yenye tint alikutana na jamaa mwenye Hammer kwenye kwenye trafic light.

Volkswagen: Oyaa gari lako lina simu?

Hammer: Ndio, we lako linayo?

Volkswagen: Yap. gari lako lina Kitanda?

Hammer: Hapana, lako je?

Volkswagen: Yap....taa zikawaka wakatimua. 

Jamaa mwenye Hammer akaona uchungu sana Kivolkswagen kiwe na kitanda gari lake halina, akaenda kufanya modification akatengeneza bonge ya kitanda, akaanza kumsaka mwenye volkswagen amkoge. Siku moja mapema akaiona Volkswagen imepaki madirisha yamefungwa, akagonga kioo, dreva wa Volkswagen akatoka.

Hammer: Unanikumbuka?

Volkswagen: Ndio kuna nini?

Hammer: Gari yangu ina dabo bed

Volkswagen: We chizi nini yaani umenitoa bafuni uniambie utumbo huo?

No comments:

Post a Comment